Monday, January 2, 2012

TAFAKARI MASOMO YA LEO JAN 2 2012

SOMO 1:YOH 2:22 -28

Wapenzi,ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni kristo? Huyo ndiye mpinga Kristo,yeye amkanae  Baba na mwana.Kila amkanae mwana,hanaye Baba,amkirie mwana anaye Baba pia.Ninyi basi,hilo mlilolisikia tangu mwanzo na likae ndani yenu,ninyi nanyi mtakaa ndani ya mwana,na ndani ya Baba.Na hii ndio ahadi aliyotuahidia,yaani uzima wa milele.Nimewaandikia haya katika habari za watu wale wanaotaka kuwapoteza.Nanyi mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha,lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote,tena ni kweli wala si uongo,na kama yalivyowafundisha habari za mambo yote,tena ni kweli wala si uongo,na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake.Na sasa watoto wadogo kaeni ndani yake,ili kusudi atakapofunuliwa,tuwe na ujasiri,wala tusiaibike mbele zake katika kuja kwake.



INJILI
Na huu ndio ushuhuda wake Yohane,Wayahudi walipotuma kwake makuhani na walawi kutoka Yerusalemu ili wamuulize,wewe u nani?Naye alikiri wala hakukana,alikiri kwamba,mimi siye Kristo wakamuuliza ni nani basi?U Eliya wewe?akasema mimi siye,Wewe U nabii yule?Akajibu la,Basi wakmwambia Unani?tuwape majibu wale waliotupeleka.Wanenaje juu ya nafsi yako?Akasema,Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani,inyosheni njia ya bwana,kama vile alivyonena nabii Isaya.Nao wale waliotumwa walikuwa wametoka kwa mafarisayo.Wakamuuliza wakamwambia ,mbona basi wabatiza,ikiwa wewe si kristo,wala Eliya wala nabii yule?Yohane akawajibu akasema,mimi nabatiza na maji.Katikati yenu amesimama yeye msiyemjua ninyi.Ndiye yule ajaye nyuma yangu,ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya kiatu chake.Hayo yalifanyika huko Bethania ng'ambo ya Yordani,alikokuwako Yohane akibatiza.

No comments:

Post a Comment