Thursday, January 12, 2012

FAUSTIN MTEGETA - HISTORIA YAKE YA UIMBAJI

                         Faustin Mtegeta(katikati) akibadilishana mawazo na walimu wenzake.

Jina ;FAUSTIN JOHN MTEGETA
Kabila ; MZIGUA
Kijiji ;PEMBA
Parokia ;MASKATI
Mkoa ;MOROGORO
Kuzaliwa ; 3/3/1963

HISTORI

    Tangu nikiwa mdogo nilianza kuimba kwaya ya shule ya msingi kama mpiga filimbi hatimaye kuwa school Band Master.Pia sikubaki nyuma katika kwaya ya kanisa,nilikuwa muimbaji wa sauti ya tatu katika kigango cha Mt.Petro hapohapo kijijini pemba parokia ya Maskati nikiwa chini ya walimu wangu wawili 1) Fr.Otto Habiri ambaye hivi sasa ni padre wa kianglikana hapahapa Dar-es-salaam,2)John Mgeda ambaye kwa hivi sasa ni marehemu mungu aiweke roho yake pema peponi , Amina.
    Baada ya kuja DSM nikawa mwanakwaya wa kigango cha Buguruni huku nikiwa mwalimu wa Jaiving  wa umoja wa vijana wa parokia ya Msimbazi hapo ilikuwa mwaka 1982-84.Mwaka 1985 rafiki yangu mkubwa aitwae Victor Ukani na Yudas Mkoba(marehemu)wakatangaza darasa la muziki  nami nikawa mmojawapo .Mwaka 1986 nikaanza kujifunza na ndipo darasa zima la watu kumi na tatu nikatoka peke yangu ndiyo nilihitimu somo hilo.Nikatunga wimbo wa majilio Njoo kwetu njoo masia,mpaka leo hii nipo katika ulimwengu huu wa muziki wa injili.

MAFANIKIO
   Nimepataa mafanikio makubwa katika muziki huu wa kwaya kwani nimepata marafiki wengi ndani na nje ya nchi.

MATATIZO
   Kila kazi haikosi matatizo lakini cha msingi ni kuyavumilia na kupambana nayo ili kazi ya Kristo mfufuka iendelee.
    Nimeoa na nina watoto wawili Innocent F.Mtegeta na Beatrice F. Mtegeta.Nawapenda sana watoto wangu.Sinywi pombe wala sikvuti sigara,namshukuru sana Mungu kwa yote hayo.

      wenu katika kristo,Faustin Mtegeta
                                                          TUMSIFU YESU KRISTO
                                                          

No comments:

Post a Comment