Monday, January 16, 2012

TAFAKARI MASOMO YA LEO,TAR.17/01/2012

SOMO  1; 1 Sam.16;1-13

        Bwana alimwambia Samweli,Hata lini utamlilia Sauli,ikiwa mimi nimemkataa asimiliki Israeli?Ijaze pembe yako mafuta,uende,nami nitakupeleka kwa Yese,Mbethlehemi;maana nimejipatia mfalmekatika wanawe.Samweli akasema nawezaje kwenda?Sauli akipata habari ataniua.Basi Bwana akasema,chukua ndama pamoja nawe,ukaseme nimekuja ili kumtolea Bwana dhabihu.Ukamwite Yese aje kwenye dhabihu,nami nitakuonyesha utakayo tenda;nawe utamtia mafuta yule nitakayemtaja kwako.Samweli akafanya hayo aliyosema Bwana,akaenda Bethlehem.Wakaja wazee wa mji kumlaki,wakitetemeka,nao wakasema;je,umekuja kwa amani?Naye akasema naam,kwa amani;nimekuja kumtolea Bwana dhabihu;jitakaseni;njooni pamoja nami kwenye dhabihu.akawatakasaYese na wanawe,akawaita kwenye dhabihu.Ikawa walipokuja,alimtakasa Eliabu,akasema,Yakini masihi wa Bwana yupo hapa mbele zake.Lakini Bwana akamwambia Samweli,usmtazame uso wake,wala urefu wa kimo chake;kwamaana mimi nimemkataa.Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo;maana wanadamu huitazama sura ya nje,bali Bwana huutazama moyo,ndipo Yese akamwita Abinadabu......

INJILI;Mk 2;23-28

   Ikawa Yesu alipokuwa akipita mashambani siku ya sabato,wanafunzi wake walianza kuendelea njiani wakivunja masuke.Mafarisayo wakamwambia,tazama,mbona wanafanya lisilokuwa halali siku ya sabato?Akawaambia,hamkusoma popote alivyofanya Daudi,alipokuwa anahaja,na kuona njaa,yeye na wenziwe?Jinsi alivyoingia katika nyumba ya mungu,zamani za kuhani mkuu Abiathari,akaila mikate ile ya wonyesho,ambayo si halali kuliwa ila Makuhani,akawapa na wenziwe?Akawaambia,sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu,si mwanadamu kwaajili ya sabato.Basi mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia.

No comments:

Post a Comment