Tanzania imepata jimbo jipya la kiaskofu,jimbo hili ni jimbo a Ifakara.Jimbo jipya la Ifakara linatokana na mgawanyiko wa jimbo la Mahenge linaloongozwa na Baba Askofu Mha.Agapitius Ndorobo.Tayari askofu mteule wa jimbo jipya la Ifakara amekwisha tajwa,naye si mwingine bali ni Baba askofu Mha.Salutarius Libena.Sherehe za kusimikwa rasmi askofu mteule(ambaye mpaka hivi sasa ni askofu msaidizi wa jimbo kuu la Dar-es-salaam)zitafanyika tar.19/03/2012.
Nikiwa ni mmojawapo wa waumini wa kutoka Ifakara,nampongeza Baba askofu Libena kwa kuteuliwa kwake,na pia waumini wote wa jimbo jipya la Ifakara kwa kupata jimbo.
No comments:
Post a Comment