SOMO 1:Sam.18:9-10,14,24-25,30-19:3
Kwa bahati Absalomu alikutana na watumishi wa Daudi.Naye Absalomu alikuwa amepanda Nyumbu akapita chini ya matawi manene ya mwaloni mkubwa hata kichwa chake kikakwama katika mwaloni huo,akanyakuliwa juu kati wa mbingu na nchi;na yule nyumbu aliyekuwa chini yake akaenda mbele.Basi mtu mmoja akaona hayo,akaenda akamwambia Yoabu,akasema,tazama,mimi.........
INJILI :Mk 5:21-43
Yesu alipokwisha kuvuka kurudi ng'ambo kataka kile chombo,wakamkusanyikia mkutano mkuu;naye alikuwa kando ya bahari.Akaja mtu mmoja katika wakuu wa sinagogi,jina lake Yairo;hata alipomwona,akaanguka miguuni pake ,akamsihi sana,akisema,Binti yangu mdogo yu katika kufa;nakuomba uje,uweke mkono waku juu yake,apate kupona na kuishi.Akaenda pamoja naye.Mkutano mkuu wakamfuata,wakimsongasonga.Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu muda wa miaka na miwili na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu wengi,amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo,kusimfae hata kidogo,bali hali yake ilizidi kuwa mbaya;aliposikia habari za yesu,alipita katika mkutano kwa nyuma,akaligusa vazi lake;akaligusa vazi lake;maana akasema,nikiyagusa mavazi yake tu,nitapona.Mara chemchemi ya damu yake ikakauka,naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule.Mara Yesu,hali akifahamu nafsini mwake kwamba nguvu zimemtoka,akageuka kati ya mkutano,akasema,ni nani aliyenigusa mavazimyangu?Wanafunzinzi wake wakamwambia,je!wawaona makutano wanavyokusongasonga,nawe wasema,ni nani aliyenigusa?Akatazama pande zote amwone ili amwone yule aliyelitenda neno hilo.Na yule mwanamke akaingiwa na hofu na kutetemeka,akajua lililompata,akaja akamwangukia,akamweleza kweli yote.Akamwambia,Binti,imani yako imekuponya,enenda zako kwa amani,uwe mzima......
No comments:
Post a Comment