SOMO 1:Sam.18:9-10,14,24-25,30-19:3
Kwa bahati Absalomu alikutana na watumishi wa Daudi.Naye Absalomu alikuwa amepanda Nyumbu akapita chini ya matawi manene ya mwaloni mkubwa hata kichwa chake kikakwama katika mwaloni huo,akanyakuliwa juu kati wa mbingu na nchi;na yule nyumbu aliyekuwa chini yake akaenda mbele.Basi mtu mmoja akaona hayo,akaenda akamwambia Yoabu,akasema,tazama,mimi.........
INJILI :Mk 5:21-43
Yesu alipokwisha kuvuka kurudi ng'ambo kataka kile chombo,wakamkusanyikia mkutano mkuu;naye alikuwa kando ya bahari.Akaja mtu mmoja katika wakuu wa sinagogi,jina lake Yairo;hata alipomwona,akaanguka miguuni pake ,akamsihi sana,akisema,Binti yangu mdogo yu katika kufa;nakuomba uje,uweke mkono waku juu yake,apate kupona na kuishi.Akaenda pamoja naye.Mkutano mkuu wakamfuata,wakimsongasonga.Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu muda wa miaka na miwili na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu wengi,amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo,kusimfae hata kidogo,bali hali yake ilizidi kuwa mbaya;aliposikia habari za yesu,alipita katika mkutano kwa nyuma,akaligusa vazi lake;akaligusa vazi lake;maana akasema,nikiyagusa mavazi yake tu,nitapona.Mara chemchemi ya damu yake ikakauka,naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule.Mara Yesu,hali akifahamu nafsini mwake kwamba nguvu zimemtoka,akageuka kati ya mkutano,akasema,ni nani aliyenigusa mavazimyangu?Wanafunzinzi wake wakamwambia,je!wawaona makutano wanavyokusongasonga,nawe wasema,ni nani aliyenigusa?Akatazama pande zote amwone ili amwone yule aliyelitenda neno hilo.Na yule mwanamke akaingiwa na hofu na kutetemeka,akajua lililompata,akaja akamwangukia,akamweleza kweli yote.Akamwambia,Binti,imani yako imekuponya,enenda zako kwa amani,uwe mzima......
Monday, January 30, 2012
HOLILI MPAKANI
Tukiwa katika mpaka wa TZ na Kenya(Holili) na wafanyakazi wenzangu wa Manispaa ya kinondoni.Toka
kushoto,Carles Mangia,Chriss Mwashusa,Arch. Alex Kampate,Omari,Eng.Uriyo,mimi mwenyewe na Daudi sigala.

Monday, January 16, 2012
TAFAKARI MASOMO YA LEO,TAR.17/01/2012
SOMO 1; 1 Sam.16;1-13
Bwana alimwambia Samweli,Hata lini utamlilia Sauli,ikiwa mimi nimemkataa asimiliki Israeli?Ijaze pembe yako mafuta,uende,nami nitakupeleka kwa Yese,Mbethlehemi;maana nimejipatia mfalmekatika wanawe.Samweli akasema nawezaje kwenda?Sauli akipata habari ataniua.Basi Bwana akasema,chukua ndama pamoja nawe,ukaseme nimekuja ili kumtolea Bwana dhabihu.Ukamwite Yese aje kwenye dhabihu,nami nitakuonyesha utakayo tenda;nawe utamtia mafuta yule nitakayemtaja kwako.Samweli akafanya hayo aliyosema Bwana,akaenda Bethlehem.Wakaja wazee wa mji kumlaki,wakitetemeka,nao wakasema;je,umekuja kwa amani?Naye akasema naam,kwa amani;nimekuja kumtolea Bwana dhabihu;jitakaseni;njooni pamoja nami kwenye dhabihu.akawatakasaYese na wanawe,akawaita kwenye dhabihu.Ikawa walipokuja,alimtakasa Eliabu,akasema,Yakini masihi wa Bwana yupo hapa mbele zake.Lakini Bwana akamwambia Samweli,usmtazame uso wake,wala urefu wa kimo chake;kwamaana mimi nimemkataa.Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo;maana wanadamu huitazama sura ya nje,bali Bwana huutazama moyo,ndipo Yese akamwita Abinadabu......
INJILI;Mk 2;23-28
Ikawa Yesu alipokuwa akipita mashambani siku ya sabato,wanafunzi wake walianza kuendelea njiani wakivunja masuke.Mafarisayo wakamwambia,tazama,mbona wanafanya lisilokuwa halali siku ya sabato?Akawaambia,hamkusoma popote alivyofanya Daudi,alipokuwa anahaja,na kuona njaa,yeye na wenziwe?Jinsi alivyoingia katika nyumba ya mungu,zamani za kuhani mkuu Abiathari,akaila mikate ile ya wonyesho,ambayo si halali kuliwa ila Makuhani,akawapa na wenziwe?Akawaambia,sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu,si mwanadamu kwaajili ya sabato.Basi mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia.

IFAKARA SASA NI JIMBO JIPYA LA KANISA KATOLIKI
Tanzania imepata jimbo jipya la kiaskofu,jimbo hili ni jimbo a Ifakara.Jimbo jipya la Ifakara linatokana na mgawanyiko wa jimbo la Mahenge linaloongozwa na Baba Askofu Mha.Agapitius Ndorobo.Tayari askofu mteule wa jimbo jipya la Ifakara amekwisha tajwa,naye si mwingine bali ni Baba askofu Mha.Salutarius Libena.Sherehe za kusimikwa rasmi askofu mteule(ambaye mpaka hivi sasa ni askofu msaidizi wa jimbo kuu la Dar-es-salaam)zitafanyika tar.19/03/2012.
Nikiwa ni mmojawapo wa waumini wa kutoka Ifakara,nampongeza Baba askofu Libena kwa kuteuliwa kwake,na pia waumini wote wa jimbo jipya la Ifakara kwa kupata jimbo.

Thursday, January 12, 2012
FAUSTIN MTEGETA - HISTORIA YAKE YA UIMBAJI
Faustin Mtegeta(katikati) akibadilishana mawazo na walimu wenzake.
Jina ;FAUSTIN JOHN MTEGETA
Kabila ; MZIGUA
Kijiji ;PEMBA
Parokia ;MASKATI
Mkoa ;MOROGORO
Kuzaliwa ; 3/3/1963
HISTORI
Tangu nikiwa mdogo nilianza kuimba kwaya ya shule ya msingi kama mpiga filimbi hatimaye kuwa school Band Master.Pia sikubaki nyuma katika kwaya ya kanisa,nilikuwa muimbaji wa sauti ya tatu katika kigango cha Mt.Petro hapohapo kijijini pemba parokia ya Maskati nikiwa chini ya walimu wangu wawili 1) Fr.Otto Habiri ambaye hivi sasa ni padre wa kianglikana hapahapa Dar-es-salaam,2)John Mgeda ambaye kwa hivi sasa ni marehemu mungu aiweke roho yake pema peponi , Amina.
Baada ya kuja DSM nikawa mwanakwaya wa kigango cha Buguruni huku nikiwa mwalimu wa Jaiving wa umoja wa vijana wa parokia ya Msimbazi hapo ilikuwa mwaka 1982-84.Mwaka 1985 rafiki yangu mkubwa aitwae Victor Ukani na Yudas Mkoba(marehemu)wakatangaza darasa la muziki nami nikawa mmojawapo .Mwaka 1986 nikaanza kujifunza na ndipo darasa zima la watu kumi na tatu nikatoka peke yangu ndiyo nilihitimu somo hilo.Nikatunga wimbo wa majilio Njoo kwetu njoo masia,mpaka leo hii nipo katika ulimwengu huu wa muziki wa injili.
MAFANIKIO
Nimepataa mafanikio makubwa katika muziki huu wa kwaya kwani nimepata marafiki wengi ndani na nje ya nchi.
MATATIZO
Kila kazi haikosi matatizo lakini cha msingi ni kuyavumilia na kupambana nayo ili kazi ya Kristo mfufuka iendelee.
Nimeoa na nina watoto wawili Innocent F.Mtegeta na Beatrice F. Mtegeta.Nawapenda sana watoto wangu.Sinywi pombe wala sikvuti sigara,namshukuru sana Mungu kwa yote hayo.
wenu katika kristo,Faustin Mtegeta
TUMSIFU YESU KRISTO

GO EAST / WEST,BUT HOME IS BEAT
Hapa ni nyumbani kwetu Ifakara eneo la Muhola,nilipokwenda kwa mapumziko mafupi hivi karibuni,hivyo vijamaa na wanangu wakifurahia mwakampya nyumbani kwao kwa ukweli.
Monday, January 2, 2012
TAFAKARI MASOMO YA LEO JAN 2 2012
SOMO 1:YOH 2:22 -28
Wapenzi,ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni kristo? Huyo ndiye mpinga Kristo,yeye amkanae Baba na mwana.Kila amkanae mwana,hanaye Baba,amkirie mwana anaye Baba pia.Ninyi basi,hilo mlilolisikia tangu mwanzo na likae ndani yenu,ninyi nanyi mtakaa ndani ya mwana,na ndani ya Baba.Na hii ndio ahadi aliyotuahidia,yaani uzima wa milele.Nimewaandikia haya katika habari za watu wale wanaotaka kuwapoteza.Nanyi mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha,lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote,tena ni kweli wala si uongo,na kama yalivyowafundisha habari za mambo yote,tena ni kweli wala si uongo,na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake.Na sasa watoto wadogo kaeni ndani yake,ili kusudi atakapofunuliwa,tuwe na ujasiri,wala tusiaibike mbele zake katika kuja kwake.
INJILI
Na huu ndio ushuhuda wake Yohane,Wayahudi walipotuma kwake makuhani na walawi kutoka Yerusalemu ili wamuulize,wewe u nani?Naye alikiri wala hakukana,alikiri kwamba,mimi siye Kristo wakamuuliza ni nani basi?U Eliya wewe?akasema mimi siye,Wewe U nabii yule?Akajibu la,Basi wakmwambia Unani?tuwape majibu wale waliotupeleka.Wanenaje juu ya nafsi yako?Akasema,Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani,inyosheni njia ya bwana,kama vile alivyonena nabii Isaya.Nao wale waliotumwa walikuwa wametoka kwa mafarisayo.Wakamuuliza wakamwambia ,mbona basi wabatiza,ikiwa wewe si kristo,wala Eliya wala nabii yule?Yohane akawajibu akasema,mimi nabatiza na maji.Katikati yenu amesimama yeye msiyemjua ninyi.Ndiye yule ajaye nyuma yangu,ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya kiatu chake.Hayo yalifanyika huko Bethania ng'ambo ya Yordani,alikokuwako Yohane akibatiza.

Subscribe to:
Posts (Atom)