Friday, October 14, 2011

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,1922-1999
Ni miaka kumi na mbili tangu mwalimu atutoke duniani.Bado tunamkumbuka mwalimu kwa mambo mengi aliyoyafanya wakati wa uhai wake,akiwa rais na hata baada ya kustaafu.Mwalimu hayupo,lakini busara na hekima zake bado zipo.Watanzania tunamkumbuka kwa mengi na hasa ushauri na maelekezo yake mbalimbali hasa juu ya maendeleo ya nchi yetu.Leo hakuna asiyekubali kuwa mwalimu alikuwa ni mtu wa aina ya pekee ambaye mwenyezi mungu alituzawadia.Mungu ailaze roho ya mwalimu mahala pema peponi.RAHA YA MILELE UMPE,NA MWANGA WA MILELE UMUANGAZIE APUMZIKE SALAMA , AMINA

No comments:

Post a Comment