Jimbo kuu la Dar-es-salaam jumamosi ya tar.26/11/2011 lilifanya sherehe za mavuno kijimbo(tegemeza jimbo) zilizofanyika katika katika viwanja vya Parokia ya Msimbazi.
Akihubiri katika misa hiyo,Mwadhama Kadinali aliwaasa watanzania kutomsahau mungu katika mambo mbalimbali yanayopanga.Alisema kuwa ipo mifano ya nchi mbalimba ambazo kutokana na maendeleo waliyokuwanayo,walimsahau mungu na kumuweka pembeni,lakini hivisasa wameanguka kiuchumi kiasi cha kuhangaika wasijue nini wafanye.
Vilevile mwadhama amewaonya watanzania juu ya kuchukua maamuzi bila ya kumshirikisha Mungu.Alisema kuwa tusidhani kuwashawishi vijana kufanya vurugu na migomo ndio dawa ya kutatua matatizo yetu.Amesema kuwa mifano ya vurugu zilizotokea Mbeya na Arusha ambazo zilitokea hivi karibuni.Amesema kuwa tunayomifano pia ya nchi zilizofanya mtindo huo wa maandmano ili kuzishinikiza serikali kutimiza madai yao lakini hata baada ya malengo yao kutimia bado vurugu hazijakoma.
No comments:
Post a Comment