Monday, November 28, 2011

MISA YA KUWAAGA MAPADRE WALIOPATA AJALI

Misa ya kuwaaga mapadre watatu wa shirika la Wakapuchi na muumini mmoja waliofariki kwa ajali ya gari Huko Ruvu mkoa wa Pwani,imefanyika siku ya Jumapili tar.28/11/2011.
   Misa hiyo iliongozwa na Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dar-es-salaam Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo,akisaidiwa na msaidizi wake Mhashabu baba askofu Salutarius Libena.Misa hii ilifanyika katika viwanja vilivypo nje ya kanisa la Pugu.
   Mapadre hao walikuwa wakitokea Dodoma kuja Dar-es-salaam.Wawili kati yao walikuwa ni wageni waliokuwa wamekuja kwa shughuli za shirika lao na walikuwa njiani kuelekea nyumbani nchini Italia.
   Misa hiyo ilihudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka hapa nchini na nje ya nchi.Serikali iliwakilishwa na Mh.Bernad Membe waziri wa mambo ya nchi za nje ambaye alimuwakilisha waziri mkuu Mh.Mizengo P.Pinda.
    Mapadre hao ni Pr.Silvio,Pr.Korado,Pr.Luciano na Andrea kijana aliyekuwanao katika safari.
    Ajali hiyo ilitokea karibu na daraja la Ruvu,baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori la mizigo.
Mungu azilazi roho za marehemu hawa mahali pema peponi AMINA

No comments:

Post a Comment