Papa Benedict XVII
Baba mtakatifu Benedict XVII anatarajiwa kutembelea Cuba na Mexico wakati wa majira ya machipuo mwakani,Vatikan imetangaza siku ya alhamisi wiki hii.Licha ya umri wake kukaribia miaka miaka 85 mwezi Aprili mwakani,baba mtakatifu anaonesha kuwa bado ananguvu na ari ya kuwtembelea wakatoliki duniani.
Wachunguzi wa mambo wansema kuwa safari zake nyingi zimekuwa zikiangalia zaidi nchi za Ulaya ili kujizuia kusafiri umbali mrefu.Aliwahi kutembelea Brazil mwaka 2007 na aliahidi kuwa atakwenda tena mwaka 2013 kwaajili ya siku ya vijana duniani.Baadae mwezi huu,Baba Mtakatifu anatarajiwa kutembelea Benin ikiwa ni safari yake ya pili barani Afrika katika kipindi cha miaka sita ya Upapa wake.Papa Yohane Paulo II aliwahi kutembelea Cuba mwaka 1998.
No comments:
Post a Comment