Misa ya kuwaaga mapadre watatu wa shirika la Wakapuchi na muumini mmoja waliofariki kwa ajali ya gari Huko Ruvu mkoa wa Pwani,imefanyika siku ya Jumapili tar.28/11/2011.
Misa hiyo iliongozwa na Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dar-es-salaam Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo,akisaidiwa na msaidizi wake Mhashabu baba askofu Salutarius Libena.Misa hii ilifanyika katika viwanja vilivypo nje ya kanisa la Pugu.
Mapadre hao walikuwa wakitokea Dodoma kuja Dar-es-salaam.Wawili kati yao walikuwa ni wageni waliokuwa wamekuja kwa shughuli za shirika lao na walikuwa njiani kuelekea nyumbani nchini Italia.
Misa hiyo ilihudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka hapa nchini na nje ya nchi.Serikali iliwakilishwa na Mh.Bernad Membe waziri wa mambo ya nchi za nje ambaye alimuwakilisha waziri mkuu Mh.Mizengo P.Pinda.
Mapadre hao ni Pr.Silvio,Pr.Korado,Pr.Luciano na Andrea kijana aliyekuwanao katika safari.
Ajali hiyo ilitokea karibu na daraja la Ruvu,baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori la mizigo.
Mungu azilazi roho za marehemu hawa mahali pema peponi AMINA
Sunday, November 27, 2011
SIKU YA MAVUNO-JIMBO KUU LA DAR-ES-SALAAM
Jimbo kuu la Dar-es-salaam jumamosi ya tar.26/11/2011 lilifanya sherehe za mavuno kijimbo(tegemeza jimbo) zilizofanyika katika katika viwanja vya Parokia ya Msimbazi.
Akihubiri katika misa hiyo,Mwadhama Kadinali aliwaasa watanzania kutomsahau mungu katika mambo mbalimbali yanayopanga.Alisema kuwa ipo mifano ya nchi mbalimba ambazo kutokana na maendeleo waliyokuwanayo,walimsahau mungu na kumuweka pembeni,lakini hivisasa wameanguka kiuchumi kiasi cha kuhangaika wasijue nini wafanye.
Vilevile mwadhama amewaonya watanzania juu ya kuchukua maamuzi bila ya kumshirikisha Mungu.Alisema kuwa tusidhani kuwashawishi vijana kufanya vurugu na migomo ndio dawa ya kutatua matatizo yetu.Amesema kuwa mifano ya vurugu zilizotokea Mbeya na Arusha ambazo zilitokea hivi karibuni.Amesema kuwa tunayomifano pia ya nchi zilizofanya mtindo huo wa maandmano ili kuzishinikiza serikali kutimiza madai yao lakini hata baada ya malengo yao kutimia bado vurugu hazijakoma.

VATICAN CITY-24 NOV-2011
Papa Benedict XVII alhamis tar.24/11/2011 amesema kuwa kumekuwa na tofauti kubwa kati ya masikini,na tofauti hiyo inazidi kuongezeka wakati huu hasa kutokana na kuyumba kwa uchumi wa nchi nyingi duniani.Ameshauri kuwa ili kuwasaidia masikini hao,haitoshi kuwasaidia kwa kuwatibu njaa iliyopo badala ya kutafuta sababu ya njaa hiyo.
Alikuwa akiongea katika mkusanyiko wa wanajumuia ya Caritas wa Italia mjini Vatican.Amesema kuwa makundi makubwa ya wahamiaji,majanga ya kiasili na vita ni mambo ambayo kwa wakati huu yamefanya kuwepo na haja ya kutolewa misaada hiyo.Mambo hayo ndiyo yanayosababisha umasikini kuongezeka kwa kiasi kikubwa.

Monday, November 14, 2011
Saturday, November 12, 2011
PAPA KUTEMBELEA CUBA/MEXICO
Papa Benedict XVII
Baba mtakatifu Benedict XVII anatarajiwa kutembelea Cuba na Mexico wakati wa majira ya machipuo mwakani,Vatikan imetangaza siku ya alhamisi wiki hii.Licha ya umri wake kukaribia miaka miaka 85 mwezi Aprili mwakani,baba mtakatifu anaonesha kuwa bado ananguvu na ari ya kuwtembelea wakatoliki duniani.
Wachunguzi wa mambo wansema kuwa safari zake nyingi zimekuwa zikiangalia zaidi nchi za Ulaya ili kujizuia kusafiri umbali mrefu.Aliwahi kutembelea Brazil mwaka 2007 na aliahidi kuwa atakwenda tena mwaka 2013 kwaajili ya siku ya vijana duniani.Baadae mwezi huu,Baba Mtakatifu anatarajiwa kutembelea Benin ikiwa ni safari yake ya pili barani Afrika katika kipindi cha miaka sita ya Upapa wake.Papa Yohane Paulo II aliwahi kutembelea Cuba mwaka 1998.

Friday, November 11, 2011
MAONI-KIFO CHA MURISHIWA
Kwa hakika nilipokea habari za kifo cha marehemu Bw.Mrishiwa kwa mshituko mkuu,mno hapa nchini Kenya.Nyimbo zake ni maarufu sana hapa na tumempoteza mkatoliki shupavu sana.Habari za kifo chake zilienea kote nchini,jinsi moto uwakavyo katika kichaka kilicho kauka nyasi.Mungu amuweke mahali pema hadi tutakapokutana tena.
Nawapongeza wanakwaya wote Tanzania kwa ushirikiano mlioonyesha na mungu awabariki.
John Githuka
Jimbo kuu katoliki-Mombasa
Kenya
Nawapongeza wanakwaya wote Tanzania kwa ushirikiano mlioonyesha na mungu awabariki.
John Githuka
Jimbo kuu katoliki-Mombasa
Kenya
ROBERT AACHANA NA UKAPERA
Bw.Robert Kilau mwanakwaya wa kwaya ya Mt.Karoli Lwanga ya parokia ya Makoka jimbo kuu la Dar -es-salaam,aliachana na ukapela jumamosi iliyopita kwa kufunga ndoa na Bi.Yusta Mwakasanga.Ndoa hiyo ilifungwa katika kanisa la Mt.Gaudence-Makoka-DSM.Ndoa hiyo walifungishwa na paroko msaidizi wa kanisa hilo Pr.Pascal Kamugisha.Pichani Robert na Yusta wakitoka nje ya kanisa baada ya kufunga ndoa.
Monday, November 7, 2011
Sunday, November 6, 2011
KWAYA YA MT.AGUSTINO-MLALAKUWA YATOA ALBAM YA KWANZA
Kwaya ya Mt. Agustino ya Mlalakuwa parokia ya Mt.Maximilian Kolbe mwenge.wamerekodi albam yao ya kwanza ambayo imezinduliwa jana katika uwanja unaotarajiwa kununuliwa kwa ajili ya matumizi ya kanisa.Albam hiyo yenye nyimbo 14 imesheheni nyimbo zilizojaa ujumbe na ni nyimbo zilizotungwa na watunzi mbalimbali hapa nchini.Nyimbo zilizopo katika albam hiyo ni;
(1)Neno la mungu (I.Mwenyasi)
(2)Kwenye raha yako(S.Mutaboyerwa)
(3)Utukufu na ukuu(Zakaria H.Kalima)
(4)Moyoni nimeonja(D.W.minja)
(5)Nipo hapa kama mtumishi(S.Mutaboyerwa)
(6)Chakula kingine ni bora(Ado)
(7)Nitakapotakaswa(Justine Ncheye)
(8)Natazama ilivyo vema(A.Nambuyu)
(9)Kwako Bwana(Gonzaga Muchunguzi)
(10)Nipe nguvu(I.Mwenyasi)
(11)Mimi ndimi nuru(E.B.Ngakuka)
(12)Nafsi yangu(F.F.Mutasingwa)
(13)Tangazeni wokovu(Emestus Ogeda)
(14)Malezi ya Watoto(Prosper Basheka)
Kinanda kimepigwa na Ernestus Ogeda
Conductor-F.F.Mutasingwa
C.D.hii inapatikana parokiani Mwenge na hivi karibuni itaanza kusanbazwa kwenye parokia mbalimbali.

Subscribe to:
Posts (Atom)