Monday, February 6, 2012

TAFAKARI,MASOMO YA LEO,JUMANNE FEB 6 2012

    Sulemani alipokusanya wazee wa Israeli,na wakuu wote wa kabila,wakuu wa mbari za mababa wa wana wa Israeli,wamwendee mfalme Sulemani huko Yerusalemu,ili walipandishe sanduku la agano l Bwana kutoka mji wa Daudi,yaani,Sayuni.Wakakutana na mfalme Sulemani watu wote wa Israeli wakuti wa sikuu,katika mwezi wa Ethanimu,ndio mwezi wa saba.Wazee wote wa Israeli wakaja,nao Makuhani wakajitwika sanduku.Wakalipandisha sanduku la Bwana,na ile hema ya kukutania,na vyombo vitakatifuvyote vilivyokuwa katika ile hema;vitu hivyo makuhani na walawi wakavipandisha.Mfalme Sulemani,na mkutano wote wa Israeli walikutanika kwake,walikuwako pamoja nae mbele ya sanduku,wakichinja sadaka kondoo na ng'ombe wasioweza kuhesabiwa wala kufahamiwa idadi yao kwa kuwa wengi.Makuhani wakalileta sanduku la agano la Bwana hata mahali pale,katika chumba cha ndani cha ile nyumba,patakatifu pa patakatifu,naam,chini ya mbawa za makerubi.Kwa maana makerubi walinyosha mbawa zaojuu ya mahali pa sanduku,makerubi wakalifunika lile sanduku na miti yake kwa juu.Hamkuwa na kitu ndani ya sanduku,ila zile mbao.....

SOMO LA 2

  Yesu na wanafunzi wake walipokwisha kuvuka,walifika nchi ya Genezareti,wakatia nanga.Nao wakiisha kutoka mashuani,mara watu walimtambua,wakaenda mbio,wakizunguka nchi ile yote,wakaanza kuwachukua vitandani walio hawawezi,kwenda kila mahali waliposikia kwamba yupo.Nkila alikokwenda,akiingia vijijini,au mijini,au mashambani,wakawaweka wagonjwa sokoni,wakamsii waguse ngaa pindo la vazi lake, nao wote waliomgusa wakapona.

Saturday, February 4, 2012

HILI NDILO ENEO LA MAGOMENI KOTA



Picha zote tatu ni eneo  zilipokuwapo kota za Magomeni ambazo zimebomolewa na kunatarajiwa kujengwa majengo ya kisasa.